Dhahabu ya Kijani: Siri ya Kushinda Soko la Parachichi Ulaya na Mashariki ya Kati (Middle East)

Picha ya Masoko ya Parachichi inayoonesha kikapu cha parachichi katika tenga au boksi la mbao, pembeni kuna bendera za Umoja wa Ulaya na Bendera ya nchi za Mashariki ya kati

Uchambuzi: Zao la Parachichi (Hass Variety) limekuwa mkombozi, lakini soko la nje lina "sheria" zake.

  1. Soko la Ulaya (EU): Hapa ndipo kuna bei kubwa, lakini vigezo ni vikali. Wanajali sana Environmental Sustainability na Social Responsibility. Unahitaji vyeti kama GlobalG.A.P na GRASP.

  2. Soko la Middle East (Dubai/Saudi): Hili soko linakua kwa kasi na ni rafiki kwa kuanzia. Wanajali zaidi muonekano, ukubwa (Size 12-18), na ladha. Safari ya kuelekea huko ni fupi (Sea freight), hivyo hatari ya kuharibika ni ndogo.

  3. Vigezo vya Msingi:

    • Mabaki ya Kemikali (MRLs): Lazima yawe chini ya kiwango kilichokubaliwa.

    • Ufungashaji: Maboksi ya 4kg ndiyo standard.

    • Traceability: Lazima uweze kueleza tunda hili limetoka shamba gani na lilitunzwa vipi.

 

Vyanzo:

  • Tanzania Horticultural Association (TAHA).

  • CBI (Centre for the Promotion of Imports from developing countries).

  • ITC (International Trade Centre) - Trade Map Data.

1 comment

Afterthought:
“Soko la nje haliitaji ‘Parachichi’, linahitaji ‘Viwango’. Ukishinda kwenye kiwango, soko litakupigania wewe badala ya wewe kupigania soko.”

Tiago, Printiago Team

Weka Maoni Yako | Leave a comment