Orodha ya Wadau na Mawakala wa kusafirisha nje ya Tanzania (Mnyororo wa parachichi)

Orodha ya Wadau na Mawakala wa kusafirisha nje ya Tanzania (Mnyororo wa parachichi)

Hawa ndio watu wa kuwafuatilia (Follow) na kuwatumia email ili kupata fursa za uwakala au masoko:

1. TAHA (Tanzania Horticultural Association)

Hili ndilo "Bunge" la wadau wa mboga na matunda. Wao wana database ya wanunuzi (Buyers) wa nje na wanajua vigezo vyote vya Dubai na Ulaya.

  • Kazi yao kwako: Kukupa miongozo ya vyeti na kukuunganisha na wakulima wakubwa.

  • Website: taha.or.tz

2. Africado Limited (Sanya Juu, Kilimanjaro)

Hawa ni miongoni mwa "Exporters" wakubwa zaidi Tanzania. Mara nyingi hufanya kazi na wakulima wadogo (Outgrowers).

  • Fursa: Unaweza kujifunza mfumo wao wa ufungashaji na namna wanavyopata oda za nje.

3. Kuza Africa

Kampuni inayojihusisha na kusaidia biashara za kilimo kufika masoko ya kimataifa. Wako vizuri sana kwenye masuala ya "Strategy."

4. Tanzania Trade Development Authority (TanTrade)

Hawa ndio wenye dhamana ya kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi. Kila mwaka huwa na ripoti za masoko mapya (Market Intelligence Reports).

5. Soko la Jebel Ali (Dubai) - Kupitia LinkedIn

Mzee wangu, hii ni mbinu ya kijasusi. Ingia LinkedIn, tafuta watu wenye vyeo vya "Produce Buyer" au "Fruit Importer" walioko Dubai au Qatar. Hapo ndipo utapata "Direct Agents" ambao wanatafuta matunda kutoka Afrika Mashariki.

 

"Je, unatamani kuanza biashara ya kuuza parachichi nje lakini hujui uanzie wapi? Weka maoni yako hapa chini au jiunge na Inner Circle yetu kupata muongozo wa hatua kwa hatua!"

0 comments

Weka Maoni Yako | Leave a comment