Fursa ya Milioni 180 kwa Startups za Afya: Hub71+ Life Sciences Inatafuta Wabunifu (Cohort 19)

Fursa ya Milioni 180 kwa Startups za Afya: Hub71+ Life Sciences Inatafuta Wabunifu (Cohort 19)

Utangulizi: Je, una startup inayojihusisha na teknolojia ya afya (HealthTech), vifaa tiba (MedTech), au kibaolojia (BioTech)? Abu Dhabi inakuitia! Programu ya Hub71+ Life Sciences imefungua milango kwa ajili ya Cohort 19, ikitafuta wabunifu kutoka kote ulimwenguni ili kuwasaidia kukuza biashara zao kufikia soko la kimataifa.

Zawadi na Faida kwa Washiriki:

Ukishachaguliwa kujiunga na mfumo huu wa kipekee wa teknolojia nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), utapata:

  • Mtaji wa Cash: Dola za Kimarekani $70,000 (zaidi ya TSh Milioni 180) kupitia mkataba wa SAFE.

  • Msaada wa Kitaalamu: Huduma na msaada wa kibiashara wenye thamani ya $70,000 nyingine (In-kind support).

  • Masoko na Mitandao: Nafasi ya kufanya kazi na mahospitali makubwa, wawekezaji, na washauri wa biashara (mentors) duniani.

  • Ufikiaji wa Soko: Fursa ya kukuza bidhaa yako kutoka maabara hadi kwa mgonjwa kupitia miundombinu ya kisasa ya Abu Dhabi.

Nani Anaruhusiwa Kuomba?

Programu hii inawalenga waasisi (founders) wenye suluhisho katika nyanja zifuatazo:

  1. Digital Health: Programu au App za kusaidia matibabu.

  2. MedTech: Vifaa vya kisasa vya tiba.

  3. BioTech: Ubunifu wa kibaolojia na madawa.

Tarehe Muhimu za Kuzingatia:

  • Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe 01 Februari, 2026.

  • Kuanza Kwa Programu: Usaili na maandalizi (onboarding) yataanza Juni 2026, na programu rasmi kuanza Septemba 2026.


Ushauri wa Printiago kwako Msomaji:

Hii ni fursa adhimu kwa vijana wa Kitanzania na Afrika Mashariki ambao mmetengeneza mifumo ya kurahisisha huduma za afya. Usiogope kuwa wazo lako ni dogo; Hub71 wanatafuta "potential" ya kukua.

Tayari kuomba? Tembelea tovuti rasmi hapa kwa maelezo zaidi na kuanza maombi yako:

👉 Hub71+ Life Sciences Application

1 comment

Tafakari ya Ziada (Afterthought):

Kabla hujaanza kutuma maombi ya Hub71, kumbuka kuwa hawaangalii tu uzuri wa wazo lako, bali wanaangalia “Scalability” (uwezo wa biashara kukua nje ya mipaka ya Tanzania).

Siri ndogo: Hakikisha kwenye maombi yako unaonyesha jinsi gani teknolojia yako inaweza kusaidia wagonjwa hata wa Abu Dhabi au nchi nyingine za Afrika. Ikiwezekana, andaa “Pitch Deck” fupi inayoonyesha timu yako na mafanikio madogo (traction) mliyopata hadi sasa. Hii itakuweka juu ya wengine!

Tiago Patrick - Printiago Team •

Weka Maoni Yako | Leave a comment