Utangulizi: Mara nyingi tunafikiri kuwa kuanza biashara lazima uwe na mamilioni benki. Ukweli ni kwamba, wafanyabiashara wengi wakubwa unaowaona leo Kariakoo au Posta, walianza kama "uchuuzi" au "uwinga." Katika mazingira ya sasa, mtaji mdogo si kikwazo cha mafanikio, bali ni mbegu ya kwanza. Ikiwa una kuanzia TSh 100,000 hadi Milioni 20, nafasi ya kujiajiri ipo wazi.
1. Uwinga na Uchuuzi: Shule ya Kwanza ya Biashara
Kuwa "winga" (dalali wa mitaani) pale Kariakoo au mchuuzi wa bidhaa ndogo ndogo si jambo la kuonea aibu. Hapa ndipo utakapojifunza siri kuu ya biashara: Saikolojia ya Mteja.
-
Mtaji: TSh 0 - 50,000 (Hapa unatumia mdomo na miguu yako tu).
-
Faida: Unatengeneza mtandao wa wauzaji wa jumla na wateja. Watu wengi wameanza kama mawinga na leo wanamiliki maduka makubwa.
2. Biashara ya Bidhaa za Msimu (Uchuuzi)
Hii inahusisha kununua bidhaa zinazopendwa kwa wakati huo na kuzisogeza kwa wateja walipo (ofisini au mitaani). Mfano: Mashuka, vyombo vya jikoni, au vifaa vya kielektroniki.
-
Mtaji: TSh 200,000 - 1,000,000.
-
Mbinu: Tumia WhatsApp Status yako kama duka. Sogeza bidhaa kwa mteja badala ya kusubiri mteja aje ofisini.
3. Huduma za Wakala (Mobile Money & Banking)
Biashara ya mawakala (M-Pesa, Mix By Yas, n.k.) bado ni mkombozi, hasa maeneo ya pembezoni mwa miji au vijijini.
-
Mtaji: TSh 2,000,000 - 10,000,000.
-
Siri ya Mafanikio: Location (eneo). Chagua eneo lenye mzunguko wa watu lakini lenye uhaba wa huduma hizo.
4. Usafiri: Pikipiki (Bodaboda) au Bajaji
Kwa kijana mwenye kuanzia Milioni 2.5 hadi 10, uwekezaji kwenye usafiri bado una tija kubwa Tanzania.
-
Mbinu: Unaweza kuajiri dereva au kujiendesha mwenyewe (Self-employed). Hii inakupa kipato cha kila siku (Daily income) ambacho kinaweza kutumika kuwekeza kwenye biashara nyingine.
5. Usambazaji wa Bidhaa za Chakula (Food Distribution)
Kununua mazao kama mchele au maharage kutoka mikoani na kuyasambaza kwenye maduka ya rejareja mijini.
-
Mtaji: TSh 5,000,000 - 20,000,000.
-
Fursa: Uhitaji wa chakula haupungui. Ukipata mashine ndogo ya kufungasha (packaging), unaongeza thamani na kuuza kwa bei ya juu zaidi.
0 comments