"Watu wengi wanafikiri lazima uwekeze (invest) ili uwe tajiri. Hiyo siyo kweli. Kutengeneza pesa ni rahisi. Kubaki na utajiri ndiyo sehemu ngumu.
Ngoja nikuonyeshe kitu ambacho kinaweza kubadili mtazamo wako wa pesa milele. Watu wawili. Uchumi mmoja. Kipindi kimoja.
Mtu A: Anaingiza shilingi 18,500,000 (milioni 18.5 za Kitanzania) kwa mwaka kama mwajiriwa.
-
Haanzishi biashara kubwa.
-
Hazingatii kuwa 'mwekezaji mtaalamu'.
-
Anastaafu akiwa na umri wa miaka 58 akiwa na utajiri wa Milioni 500.
Mtu B: Anaingiza 55,500,000 (milioni 56) kwa mwaka (mara tatu ya Mtu A).
-
Anafanya kazi hadi anaumri wa miaka 70.
-
Anakufa akiwa hana kitu (broke).
Tofauti ni nini? Mtu A alijua 'Ujanja' (The Trick). Mtu B hakuujua hilo. Na ujanja huo siyo mgumu, ni utofauti tu huo mdogo.
Ujanja siyo kiasi gani unatengeneza; kila mtu anaweza kutengeneza pesa. Ujanja ni nini unakifanya na pesa yako mara tu inapoingia kwenye akaunti yako.
Mtu B alifanya hivi (kama wafanyavyo wengi):
-
Mshahara unaingia.
-
Kodi inachukua fungu kubwa.
-
Kinachobaki kinaenda kwenye 'Akiba' ('Savings').
-
Akiba (au Savings kwa kimombo) inapata faida ya 1% wakati mfumuko wa bei (inflation kwa kimombo) upo 7-8%.
-
Anafanya kazi kwa bidii zaidi.
-
Anaingiza zaidi.
-
Anazidi kuwa bize.
-
Baada ya miaka 30? Bado hajui pesa yake inapaswa kuelekea wapi.
Mtu A alifanya tofauti: Mtu A alijifunza kuwa kuna maeneo sita (6) ambapo pesa yako inapaswa kuelekea haraka sana baada ya kuipata. Siyo kwenye akaunti za akiba, siyo kwenye mifumo ya kawaida ya kustaafu. Ni hatua 6 mahususi zinazolinda pesa dhidi ya:
-
Mfumuko wa bei (Inflation).
-
Serikali kuchapa pesa hovyo.
-
Kuporomoka kwa soko.
-
Vurugu za kiuchumi.
Mtu A alijifunza hili akiwa na miaka 35... na hakuwahi kuwa na wasiwasi na pesa tena.
Mtu B alitengeneza pesa mara nne zaidi, alifanya kazi mara mbili zaidi, lakini bado alijiuliza, 'Hizi pesa zote zimeenda wapi?' Huu ndiyo uwezo wa kujua ujanja. Huhitaji kuacha kazi, huhitaji kuanza biashara. Unahitaji tu kujua kile Mtu A alichokijua."

UCHAMBUZI WA PRINTIAGO: UNAMALIZAJE MWAKA WAKO WA 2026?
Mtu wangu wa nguvu, hii makala ni kioo kwa kila mjasiriamali na yule ambae bado hajaanza ujasiriamali. Hapa ndipo tunapofeli:
1. Mtego wa "Mshahara Mkubwa" (The Income Trap)
Tanzania tuna vijana wengi wanafanya kazi mashirika makubwa au miradi mikubwa (Madini, makampuni ya mawasiliano na ya kifedha, taasisi au kampuni za kiserekali na binafsi) na wanapata mishahara minono (Kama Mtu B). Wanakula bata, wananunua magari ya kifahari, lakini akaunti iko tupu.
-
Somo: Usijisifu kwa kuingiza milioni 10 kwa mwezi kama hujui hiyo milioni 10 inaenda wapi hilo ni tatizo.
2. Akiba (Savings) ni Hasara
Kiyosaki anasema kuweka pesa benki (Savings) wakati mfumuko wa bei (au inflation) unapanda ni kupoteza pesa. Ukishika TSh 1,000,000 (Milioni 1) leo, baada ya mwaka mmoja thamani yake itakuwa imeshuka.
-
Somo: Pesa lazima "iegeshwe" (Parked) kwenye rasilimali zinazopanda thamani (Assets) kuliko mfumuko wa bei.
3. Maeneo 6 ya Kiyosaki (Zingatia vitu hivi 6)
Ingawa Kiyosaki anauza "Playbook" yake, maeneo haya kwa mazingira yetu mara nyingi ni:
-
Dhahabu/Fedha (Gold/Silver): Kulinda thamani.
-
Ardhi/Real Estate: Inayozalisha kodi (Rent).
-
Biashara (Systems): Inayojiendesha bila wewe kuwepo
-
Elimu ya Kifedha: Kujua sheria za kodi na sheria za nchi.
-
Bitcoin/Digital Assets: (Kwa sasa hivi ndiyo habari ya mjini kwa ajili ya kukwepa mfumuko wa bei).
-
Cashflow Commodities: Vitu vinavyohitajika kila siku (chakula, nishati).
Vyanzo: * Robert Kiyosaki Official page(Facebook/Twitter). * Rich Dad Poor Dad Philosophy (Falsafa za baba zangu wapendwa tajiri na maskini).
1 comment
Afterthought:
“Pesa ni kama maji; usipoitengenezea mfereji (system) wa kuelekea unakotaka, itazama ardhini au itatiririka kwenda kwa watu wengine. Swali siyo kiasi gani umeingiza leo, swali ni: Je, pesa uliyoingiza leo itakuwa bado inakufanyia kazi miaka 20 ijayo?”