|
UTANGULIZI:
Wengi wetu tunapoanza biashara, swali la kwanza tunalojiuliza ni: "Nitapata wapi pesa?" Lakini kwa bilionea Strive Masiyiwa, hili ni swali la makosa. Katika darasa lake la kipekee kwa vijana wa Afrika, anasema siri ya utajiri haipo kwenye kuwaza pesa, bali kwenye kuangalia mazingira yanayokuzunguka.
|
-
-
Kitambulisho cha Mjasiriamali ni Suluhisho/Tiba ya Tatizo ("Solution" kwa kiingereza)Masiyiwa anasisitiza kuwa ukiwa mjasiriamali, kazi yako si kuuza bidhaa tu, bali ni kutatua changamoto. "Kuna matatizo mengi yanatuzunguka Afrika: umeme, maji, usafiri, na chakula. Kila tatizo unaloliona ni fursa ya biashara iliyojificha," anasema. Ukishatatua tatizo la watu, pesa itakufuata yenyewe.
-
Anza na Kidogo Ulichonacho (Start Small)
Masiyiwa anakumbusha namna alivyoanza biashara yake ya kwanza ya ujenzi na baadaye Econet. Hakusubiri mabilioni. Anashauri vijana kuanza na kile walichonacho mkononi. Uaminifu (Integrity) ndio mtaji mkuu kuliko fedha za benki.
-
Kanuni ya Imani & Kujituma ("Faith and Hardwork")
Huwezi kufika mbali ukiwa mvivu. Strive anasema nidhamu ya kazi ndiyo inayotofautisha waliofanikiwa na wanaoota tu kufanikiwa. Lazima uwe tayari kufanya kazi saa nyingi zaidi ya mfanyakazi wa kawaida.
-
Jenga Sifa (Reputation) Kabla ya Utajiri
"Jina lako ni muhimu kuliko akaunti yako ya benki," anasema Masiyiwa. Katika biashara, uaminifu ndio utakaokufanya upate washirika (partners) na wawekezaji. Ukidanganya mara moja, umechoma daraja la mafanikio yako ya baadaye.
|
| Chanzo cha Taarifa (Source): Makala hii imechambuliwa kutoka kwenye mfululizo wa masomo ya "Strive Masiyiwa kwenye page yake rasmi ya Facebook " (masomo ya mfululizo yaliyojulikana kama Afterthought), hasa somo lake la tarehe 15 Oktoba 2018, ambapo alizungumzia kwa kina kuhusu "Identifying Opportunities in Africa." Strive amekuwa akitumia ukurasa wake wa Facebook kama jukwaa kuu la "Mentorship" kwa zaidi ya miaka 10 sasa |
Ushauri wa Printiago kwako Msomaji:
Unapotazama mtaa wako wa Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kigali au Nairobi leo; ni tatizo gani dogo ambalo ukilitatua leo, watu watakuwa tayari kukulipa? Hapo ndipo safari yako ya ubilionea inapoanzia.
Tukutane kwenye komenti hapo chini.
1 comment
Tafakari ya Ziada (Afterthought):
Unajua kwanini Masiyiwa anasisitiza sana kuanza na ulichonacho? Ni kwa sababu “Mtaji wa Akili” huwa haufilisiki. Watu wengi wanasubiri mkopo wa benki ili waanze, lakini benki huwa hazikopeshi “mawazo,” zinakopesha “mizunguko ya pesa” (cashflow).
Ukianza leo kwa kutatua tatizo dogo mtaani kwako kwa kutumia laki moja, unatengeneza historia ya kibiashara ambayo kesho itamshawishi mwekezaji au benki kukuamini na mamilioni. Usidharau mwanzo mdogo; dharau kukaa bila kuanza.