Utangulizi: Watu wengi wanahangaika kifedha maisha yao yote kwa sababu moja rahisi: Hawajui tofauti kati ya Asset (Rasilimali) na Liability (Deni/Gharama). "Baba yangu Tajiri" (Rich Dad) aliniambia, "Kama unataka kuwa tajiri, lazima ujifunze kusoma namba na uelewe tofauti ya vitu hivi viwili." Shuleni tunafundishwa jinsi ya kufanya kazi ili kupata pesa, lakini hatufundishwi jinsi ya kuzifanya pesa zitufanyie kazi.
1. Asset (Rasilimali) ni nini?
Kwa lugha rahisi, Asset ni kitu chochote kinachoweka pesa mfukoni mwako. Haijalishi unajisikiaje kuhusu kitu hicho, kama hakileti faida ya kifedha kila mwezi, hicho siyo Asset.
-
Mifano ya Assets: Nyumba ya kupangisha (inayoingiza kodi), biashara inayojiendesha bila wewe kuwepo, hisa (stocks) zinazotoa gawio, au hati fungani (bonds).
2. Liability (Deni/Gharama) ni nini?
Liability ni kitu chochote kinachotoa pesa mfukoni mwako. Hapa ndipo watu wengi wanapofeli. Wanafikiri wanamiliki Assets, kumbe wanamiliki Liabilities zinazowanyonya damu kila siku.
-
Mifano ya Liabilities: Mkopo wa gari la kifahari, kadi za mkopo (credit cards), na hata ile nyumba unayoishi (kama unalipia umeme, maji, na kodi bila kuingiza kipato).
Mtego wa Nyumba Unayoishi
Watu wengi husema, "Nyumba yangu ndiyo Asset yangu kubwa zaidi." Baba yangu Tajiri alikuwa anacheka na kusema, "Kama nyumba yako inatoa pesa mfukoni mwako kila mwezi, hiyo ni Liability."
Asset ya kweli ni ile nyumba ambayo mpangaji anakulipa kodi, na baada ya kulipia gharama zote, unabakiwa na faida (Cash Flow).
Siri ya Matajiri vs. Maskini
-
Maskini: Wana gharama nyingi kuliko kipato.
-
Tabaka la Kati (Middle Class): Wanannua Liabilities wakifikiri ni Assets (kama magari mapya na mikopo ya nyumba).
-
Matajiri: Wanajenga safu ya Assets kwanza, kisha Assets hizo ndizo zinakuja kuwalipia anasa zao.
Neno la Kiyosaki: "Matajiri hununua Assets mwisho, maskini na tabaka la kati hununua Liabilities kwanza."
Hatua ya Kuchukua Leo:
Angalia orodha ya vitu unavyomiliki. Je, ni vingapi vinaweka pesa mfukoni mwako leo? Kama huna Asset hata moja, umeanza mwaka kwa hatari. Anza kidogo kidogo, jifunze kuhusu uwekezaji, na uache kununua vitu ili uonekane tajiri wakati huna Cash Flow.
0 comments